DIWANI LUJUO AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU KATA YA BOMA.
DIWANI wa Kata ya Boma Manispaa ya Morogoro,Mhe. Athuman Lujuo, ameahidi kutatua changamoto za elimu zinazoikumba shule zake zilizopo Kata ya Boma ikiwamo shule ya Sekondari Tubuyu ambayo kuna changamoto za uchakavu wa sakafu ya madarasa pamoja na uchakavu wa ubao wa kufundishia.
Kauli hiyo ameitoa mapema
Desemba 17/2021 , wakati alipokua katika ziara ya siku moja ya kukagua
miundombinu ya shule zilizopo Kata ya Boma ambapo katika Shule ya Sekondari Tubuyu
amekuta madarasa manne (4) sakafu
imechakaa na kuharibika na madarasa matatu (3) ubao wa kufundishia umechakaa.
Akizungumza juu ya ziara yake, Mhe. Lujuo,amesema kuwa kwa sasa
jukumu kubwa ni kuhakikisha Kata ya Boma inapiga hatua katika Nyanja zote.
“Changamoto kubwa ambazo
nimeziona na tunazo katika Kata yetu ya Boma hususani katika Sekta ya elimu ni
uchache wa vyumba vya madarasa, uchakavu wa sakafu na mabati, uhaba wa vifaa
vya kufundishia, uchakavu wa ubaoa wa kufundishia pamoja na uahaba wa vyumba za
Waalimu, katika kuona hizi changamoto zinatatuliwa , nitahakikisha changamoto
zinazozikabili shule zetu zilizopo Kata yetu ya Boma ninazitatua kwa kutumia
nguvu zangu binafsi kama Diwani kwani kitendo cha wananchi kunichagua
kimeonesha kuwa na Imani na mimi , hivyo nina kila sababu ya kuhakikisha
changamoto za shule hizi nazitatua kwa haraka kipndi hiki ambacho wanafunzi
wapo likizo ili wakifungua shule wakute mazingira mazuri na arafiki kwa kusoma”
Amesema Mhe. Lujuo.
Mhe. Lujuo, amesema kuwepo kwa mazingira ambayo sio rafiki
shule ni moja ya sababu ambayo inaweza
kuwapelekea wanafunzi kutofanya vizuri katika masomo yao.
Katika hatua nyengine, Mhe.Lujuo, alipata nafasi ya kukagua ujenzi wa madarasa yanayojengwa chini ya moango wa UVIKO-19 katika Shule ya Sekondari Morogoro na kuridhishwa na kazi inayoendelea huku akiwataka mafundi kuafnya kazi usiku na mchana ili kukabidhi mradi huo kwa wakati.
Hata hivyo mara baada ya kuona madarasa hayo ,
amempongeza Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha za
ujenzi wa madarasa hayo huku akiwataka walimu, Wazazi kuhakikisha
wanashirikiana kikamilifu ili kuongeza ufaulu katika Shule hiyo.
Amesema, moja ya jukumu Kuu la Afisa elimu Kata
ni katika ufuatiliaji wa maendeleo ya shule za msingi na
sekondari za serikali pamoja na shule za watu binafsi zilizopo katika Kata ya
Boma katika kuona ubora wa taaluma
unakuwa wakiwango cha juu.
Katika kuona hilo la ufaulu kwa Kata yake linafanikiwa, amemuagiza amemugiza Afisa Elimu Kata ya Boma, kuhakikisha anafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa shule za Msingi na Sekondari ili mapungufu yanayobainika yaweze kufanyiwa kazi kwa wakati kwa ajili ya kuboresha taaluma shuleni na ufaulu wa wanafunzi.
Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Boma, Prisca Mawala, amemshukuru sana, Mhe. Lujuo, kwa kwenda kuwatembea shule hizo kwani anaona ziara hiyo itazaa matunda kwa kutatua baadhi ya changamoto zao ambazo zimekua zikizikabili shule hizo hususani shule ya Sekondari Tubuyu.
Post a Comment