Header Ads

KAMATI YA SIASA KATA YA BOMA YAMPONGEZA DIWANI LUJUO KUCHANGIA MIRADI YA ELIMU .



Diwani wa Kata ya Boma, Mhe. Athumani Lujuo,( kulia) akiwa na Kamati ya Siasa  wakikagua ujenzi wa Madarasa.

Msingi wa ujenzi wa darasa 1 Shule ya Msingi Bungo.

Ujenzi wa vyumba 7 vya Madarasa Shule ya Msingi Mchikichini A.

KAMATI ya Siasa Kata ya Boma, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama CCM Kata ya Boma, Ndg. Salumu Msumi, imempongeza Diwani wa Kata ya Boma Mhe. Athumani Lujuo kwa kujitoa katika kuchangia miradi ya elimu .

Pongezi hizo zimetolewa Leo Desemba 22/2021 wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa Kata ya Boma ya Kutembelea miradi ya Shule.

Akizungumza katika Ziara hiyo, Ndg. Msumi,amesema Kitendo Cha Diwani Lujuo kutumia fedha zake kushughulika na changamoto za elimu ni Jambo la kuigwa kwa Viongozi wengine kwani ameonesha jinsi gani anataka matokeo chanya ya ufaulu katika Kata yake.

" Tunampongeza Sana Diwani, tumeona Shule ya Msingi Mchikichini A amejenga madarasa 5 kwa fedha zake, na 2 nguvu za Wananchi, hili ni Jambo la kupongezwa Sana, ametumia fedha zake za kula na familia yake kwa kuwekeza katika elimu tunampongeza Sana na Wananchi wanakila sababu ya kujipongeza kupata Diwani mwenye uthubutu wa kujitoa lakini wampe ushirikiano ili afanye makubwa zaidi ya haya" Amesema Msumi.

Naye Katibu wa CCM Kata ya Boma, Ndg. Mohamed Thabiti, amempongeza Diwani pamoja na Uongozi wa Kata kwa jitihada za kusimamia miradi ya Maendeleo hususani ujenzi wa madarasa katika kuwajengea Mazingira rafiki wanafunzi kusoma vizuri na kuongeza ufaulu.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Boma ,Mhe. Athumani Lujuo, ameishukuru Kamati ya Siasa kwa kuona umuhimu wa kukagua miradi ya Kata hiyo huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa Chama kwani wao ndio watekelezaji wa Ilani ambayo inasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi CCM.

" Leo tulikuwa na ugeni wa Kamati ya Siasa Kata ya Boma, tumefarijika kupata ugeni huu, haya tunayoyafanya ni moja ya Utekelezaji wa Ilani, hivyo ujio wao ni kuona Ilani ya CCM inatekelezwa kwa vitendo na wamepongeza miradi yetu Jambo ambalo limetupa faraja na Hali ya kufanya kazi zaidi kikubwa tunawaahudi kushirikiana nao bega kwa bega katika kufanikisha ilani inatekelezwa na maendeleo yanaonekana " Amesema Mhe. Lujuo.

Aidha, Mhe. Lujuo, amesema ameamua kuanza ziara ili kuendelea kutatua Kero za Wananchi na kuona Kata ya Boma unakuwa miongoni mwa Kata zenye Maendeleo makubwa.

Katika hatua nyengine, amempongeza Mtendaji wa Kata ya Boma, Prisca Mawala, kwa usimamizi mzuri wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mzigila unaogharimu kiasi Cha Shilingi milioni 20 ambapo mpaka Sasa ujenzi huo umetumia Shilingi Milioni 10.

Miongoni mwa Shule zilizo tembelewa na Kamati ya Siasa ni pamoja Ujenzi wa vyumba 7 vya madarasa Shule ya Msingi Mchikichini A, ujenzi wa Darasa 1 Shule ya Msingi Bungo, Ujenzi wa Madarasa ya UVIKO-19 katika Shule ya Sekondari Morogoro na ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya ghorofa ya Boma.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.