MANISPAA YA MOROGORO YAKABIDHI MADAWATI 688 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 50 KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Bakari Msulwa (kulia) akipeana mkono na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kihonda mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji wa madawati .
Meza za Wanafunzi.
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro, Dkt Janeth Barongo akisoma taarifa fupi ya ugawaji wa madawati mbele ya Mkuu wa Wilaya .
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John, akisalimiana na Waalmu waliofika katika hafla fupi ya ugawaji wa Madawati.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, akizungumza na Waalimu waliojitokeza katika hafla fupi ya ugawaji wa Madawati yaliyonunuliwa kwa mapato ya ndani kwa Shule za Msingi na Sekondari Manispaa ya Morogoro.
Viti vya wanafunzi.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imekabidhi jumla ya Madawati 688 yenye thamani ya Shilingi milioni 50 kupitia makusanyo ya fedha za ndani .
Tukio hilo la kukabidhi Madawati hayo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro , Mhe. Bakari Msulwa, Agosti 24,2020 katika Shule ya Sekondari ya Kihonda iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi Madawati hayo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, alisema kuwa lengo la kutoa madawati hayo ni pamoja ya njia ya kutaka kuimarisha na kuinua viwango vya ufaulu katika Manispaa hiyo kwa kuwatengenezea mazingira mazuri wanafunzi.
“”Nawapongeza sana Manispaa ya Morogoro japo kuna changamoto ya upungufu wa madarasa, madawati, vitendea kazi, mazingira ya shule , pamoja na upungufu wa Waalimu japo kunatofautiana sna kati ya Vijijini na hapa Manispaa , Lakini Uongozi wa Manispaa ya Morogoro una maono makubwa mno, hakuna kitu kibaya katika Taifa lolote kukawa kuna mpangilio mbaya ambapo kutakuwa hakuna uwekezaji hususani katika suala la elimu na hilo Taifa likaendelea , kwahiyo hakuna Taifa duniani linaloendelea bila kuwekeza katika elimu, tunapoona Viongozi wanawekeza katika elimu basi tunaona kuna Viongozi wanaofikiria Taifa la leo na la kesho, “Amesema DC Msulwa.
“”Ndugu zangu kuna kazi nyengine kupima matokeo ni rahisi, maana ukiwa mkulima utapanda, utalima, na tutajua kiwango ulichovuna, lakini kuna kazi nyengine ambazo matokeo yake ni magumu kuyapima hivyo hivyo kwa ualimu pia matokeo yake ni rahisi kuyapima kwahiyo kila mtu ajipime katika sehemu yake tukianza elimu msingi na Sekondari je wingi wetu unaleta tija? Niwaombe walimu na kamati zenu mjipange katika kuondoa aibu ya kupata matokeo mabaya na kuhakikisha mnazalisha matokeo chanya ya ufaulu kwa wanafunzi wetu , tunapolinganishwa na Mikoa mingine na Wilaya nyengine na matokeo yetu yakawa ni mabaya ni jambo ambalo halipendezi na aibu kubwa kwani tunao wataalamu wengi na wenye uwezo mkubwa sana “Ameongeza DC Msulwa.
DC Msulwa, amezitaka Kamati za Shule zikae chini na kuweka mikakati mizuri na kijiendesha kisayansi kutokana na kuwa na wasomi ndani yake na wazazi wenye uelewa , kwani wakitegemea Manispaa imalize matatizo ya Madawati ni kujicheleweshea maendeleo katika shule zao .
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, katika kukabiliana na upungufu wa madawati, Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani ilitenga kiasi cha Shilingi milioni 50 kwa ajili ya kununua madawati katika shule za Msingi na Sekondari.
Waluse alisema katika kuhakikisha viwango vya ufaulu vinaongezeka Manispaa ya Morogoro, watahakikisha viwango vya ufaulu katika elimu msingi vinafika asilimia 90 na Sekondari asilimia 92.
“Tumejipanga vizuri sana, mpaka sasa tuna kamati yenye Wajumbe 17 na kamati hiyo ilishashuka hadi kwenye ngazi za Shule na tulishakaa kikao kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuongeza viwango vya ufaulu, mkakati wetu wa kwanza ilikuwa ni kuongeza vitendea kazi kama madawati lakini pia zaidi kufikisha ujembe kwa jamii kushiriki katika kuleta maendeleo ya ufaulu kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za shule “ Amesema Waluse.
Kwa upande wa Afisa Elimu Sekondari, Dr Janeth Barongo, katika taarifa yake ya madawati, alisema kuwa idara ya elimu ina jumla ya shule 64 za Msingi na shule 23 za Sekondari zinazomilikiwa na Serikali.
Dr Barongo,alisema kuwa shule za msingi zinawanafunzi 64,990 , wavulana 32,493 na wasichana 32497 ambapo katika upande wa Shule za Sekondari ni wanafunzi 21,186 , ikiwamo wavulana 9,616 na wasichana 11,570.
Hata hivyo, alisema kuwa elimu smingi ina mahitaji ya madawati 22,181 na yaliyopo ni 14,850 na upungufu ni 7,331, na kwa sekondari ina mahitaji ya meza ni 21, 186, na zilizopo ni 15,965 na upungufu 5,221 ambapo kwa upande wa viti mahitaji 21,186 vilivyopo ni 16, 298 na upungufu ni 4,888.
Miongoni mwa shule za msingi na Sekondari zilizopata mgao wa madawati ni pamoja na Lukobe 150, Kilongo 50, Mkundi 50, Nanenane 50, Kasanga 50, Muungano 50, Mtawala 50, Kihonda 50,Lupanga 55, Kihonda 80 pamoja na Kauzeni 53.
Post a Comment