Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO YATOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA MZEE SUDI KUFUATIA KUUNGULIWA NA NYUMBA.

 

Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias, (kushoto), akikabidhi msaada kwa Mzee Sudi Ally aliyeunguliwa na Nyumba 

fisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias, (kushoto),(anayemfuatia), Mtendaji wa Kata ya Uwanja wa Taifa, Sekela Konga, Mzee Sudi Ally (katikati) wajumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kanisani na Mratibu wa Maafa Manispaa ya Morogoro , Elizabeth Badi (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa Vyakula .








Mali zilizoteketea kwa moto.

Mratibu wa Maafa Manispaa ya Morogoro akiteta jambo na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kanisani Kata ya Uwanja wa Taifa leo mara baada y zoezi la ukabidhiwaji wa msaada wa Mzee Sudi Ally kumalizika.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro leo imeungana na Mzee Sudi Ally Mkazi wa Mtaa wa Kanisani Kata ya Uwanja wa Taifa Manispaa ya Morogoro katika kumpa mkono wa pole kufuatia kuunguliwa na Nyumba pamoja na vitu vyake .

Tukio hilo limefanyika leo Agosti 13,2020, Nyumbani kwa ,Mzee Sudi, mara baada ya Mratibu wa Maafa Manispaa ya Morogoro akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogor pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro kufika katike eneo ambalo limetokea maafa ya Moto.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mratibu wa Maafa Manispaa ya Morogoro, Elizabeth Badi, amesema lengo la msaada huo ni kumtia nguvu na kumfariji katika kipindi hiki kigumu anachopitia mzee huyo kutokana na kuunguliwa na Moto.

“”Nipo hapa nikiwa mratibu wa Maafa Manispaa ya Morogoro  lakini nimemwakilisha Mkurugenzi wetu wa Manispaa ya Morogoro kutokana na majukumu aliyonayo, lakini nipende kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Mkurugenzi nitoe pole kwa familia ya Mzee Sudi, hili  ni janga kubwa sana, na madhara makubwa ameyapata mzee wetu  huyu, tumeona tufike na kumfariji ili aweze kukidhi mahitaji yake  katika kipindi hiki cha mpito, Mkurugenzi wetu amenituma nitoe pole hizi kwa niaba yake na tupo pamoja kwa kila jambo linaloendea “Amesema Elizabeth.

Aidha, amewasaa Wananchi watoe taarifa kwa Jeshi la zima moto kipindi wanapoona kuna dalili ya hatari ya moto au maafa ya aina yoyote ikiwemo na kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya  mifumo ya waya za umeme ili kuzuia maafa yasiendelee kutokea  zaidi.

Kwa upande wa Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias, amesema Manispaa ya Morogoro imekuwa ikijali ustawi wa watu hivyo kwa msaada ambao Manispaa imeutoa kwa Mzee Sadi ni dhahiri kwamba suala la ustawi limezingatiwa na wataendelea kuwa pamoja kwa kila jambo na familia ya Mzee Sadi na watu wengine kwa ujumla katika kukuza ustawi wa Wananchi wa Manispaa ya Morogoro.

Naye, Mzee Sadi, ambaye ni muhanga wa kuunguliwa Nyumba, ameushukuru Uongozi wa Manispaa ya Morogoro chini ya Mkurugenzi wa Manispaa kwa kuonesha upendo mkubwa wa kuwajali  Wananchi wake.

“”Hili ni jambo la kipekee sana, naushukuru Uongozi wa Manispaa ya Morogoro ukiongozwa na Mkurugenzi wetu , hakika tumepata mwanga mkubwa wa hiki tulichopewa , asiyeridhika na kidogo hata kikubwa hawezi kuridhika, tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu Mkurugenzi wetu awe na afya bora na Moyo wa  kuwakumbuka Wananchi wake , lakini asichoke kutupokea tutakapo kwama tutaomba sana msaada kupitia Ofisi ya Mkurugenzi sasa hivi tunatanga tanga pa kulala tunaishi kwa ndugu lakini safari hii iliyoanzishwa tunaamini tutarejea katika hali ya kawaida” Amesema Mzee Sudi.

Miongoni mwa msaada wa  vyakula vilivyotolewa na Manispaa ya Morogoro kwa Mzee Sudi ni pamoja na Mchele kilo 30, ngano kilo 25, Unga wa Sembe kilo 25, Mharage kilo 5, Sukari kilo 5, mafuta ya kula lita 5 , na Godoro la nchi 5 kwa 6 ikiwemo na kiasi cha fedha Shilingi 50,000/= kwa ajili ya kupooza ugumu wa maisha katika kipindi hiki kifupi cha mpito.

 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.