Header Ads

RC SANARE AONGOZA MAMIA YA WATU KUMBUKUMBU YA WAHANGA AJALI YA MOTO MSAMVU.

 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare akisalimiana na mmoja wa wahanga wa ajali ya Moto aliyenusurika .

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare, akiweka shada katika Mnara wa Makaburi ya Wahanga wa ajaili ya Moto Msamvu.

Ndugu, Jamaa na Marafiki waliohudhuria kwenye Makaburi ya Kola katika kumbukumbu ya Wahanga wa ajali ya Moto Msamvu. 


Mkurugenzi Manispa aya Morogoro, Sheilla Lukuba, akiongoza msafara katika ukaguzi wa Ujenzi wa Makaburi ya Wahanga wa ajali ya Moto Msamvu katika Makaburi ya Kola Manispaa ya Morgoro.


Aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga (kushoto) akiwa na Diwani Mstaafu wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana wakiweka shada katika Mnara wa Wahanga wa ajali ya Moto Msamvu katika Makaburi ya Kola.


MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare  pamoja na viongozi wengine waongoza mamia ya watanzania waliojitokeza kwenye Makaburi  ya kola katika siku ya kumbukizi ya wahanga wa ajili ya moto iliyotokea  Tarehe 10/08/2019 Msamvu Manispaa ya Morogoro.

Tukio hilo la kumbukizi ya Wahanga wa ajali ya Moto limefanyika leo Agosti 10, 2020 kwenye Makaburi ya Kola Kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari, amewataka Wananchi kila mmoja kuwa na wajibu wa kuhakikisha anaendelea kuchukua tahadhari kwa kiala kiashiiria cha hatari kinachoweza kupoteza maisha ya watu.

RC Sanare, ameviagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama, vyombo vinavyohusika na uokoaji na majanga kuendelea kusimamia taratibu za kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za haraka pale linapotokea tatizo lolote linalofanana na janga kama lililowakumba wananchi waliopoteza maisha yao Msamvu.

Aidha, ameendelea kuvitaka Vyombo hivyo tajwa hapo juu kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi , Taasisi na Mashirika juu za hatua madhubuti za kukabiliana na Majanga kama hayo yaliyotokea .

Amesema , Serikali iliweza kuratibu na kusimamia matibabu ya waathirika wote waliopatwa na tatizo hilo ikiwa ni pamoja huduma za Kimatibabu kwa wale waliotibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na wale waliopewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

"Wakati Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, tarehe 10,03,2020 alivyotembelea makaburi haya , alitoa maelekezo ya kuhakikisha kila tarehe 10 mwezi Agosti ya kila mwaka iwe inafanyika kumbukumbu ya kuwakumbuka marehemu , alituelekeza kuwa kuhakikisha sehemu ya makaburi inatengenezwa vizuri na kuwa na mandhari ambayo wageni, ndugu na marafiki wakija kwa ajili ya kutembelea basi waone kuwa marehemu hawa wametendewa haki , kwahiyo Serikali kushirikiana na wadau imejitahidi katika hatua mbalimbali za kuhakikisha marehemu hawa wanathaminiwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa eneo hili la kuweka ukuta, Mnara wa majina kwa ajili ya kumbukumbu pamoja na kujengea kaburi moja moja , niwaombe nyote mlioshiriki katika kumbukumbu hii kuendelea kushikamana pamoja kama Taifa katika kuwaenzi wale wote waliotangulia mbele za haki " Amesema RC Sanare.

Aidha, amewashukuru Wananchi wote waliojitokeza kushirikiana na Serikali katika hatua zote ambazo zilikuwa zinachukuliwa kuhakikisha marehemu hawa wanatendewa haki.

Katika hatua nyengine , amewataka wale wote wanaohusika na Ujenzi wa Makaburi hayo wahakikishe kazi hiyo inakamilika kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati huku akiagiza Kamati ya Maafa ya Wilaya kuendelea kusimamia na kuratibu mpango wa kuzuia majanga na kuchukua hatua za kukabiliana nayo pindi yanapotokea na kuhakikisha eneo hilo linaendelea kutunzwa na linakuwa salama wakati wote.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amesema siku ya Agsoti 10, iliacha machungu makubwa na majeraha hivyo anaipongeza Serikali kwa kulifanya tukio hilo kuinga katika historia ya matukio makubwa ya majanga hapa nchini kwa ajili ya kuwakumbuka waliotangulia mbele za haki.

"Nipende kutoa salamu zangu kwa  Wananchi wa Wilaya ya Morogoro laki takribani nchi nzima  wanafuatilia tukio hilo lia kihistoria kabisa katika Mkoa wetu, jambo hili Mkuu wa Mkoa lilitugusa sana, mimi wakati ajali inatokea nilikuwepo nikawa naripoti kwa nafasi nyengine ya  Mwandishi wa habari wa TBC,kilikuwa kipindi kigumu sana kwetu na ndugu waliopoteza wapendwa wao , sisi tulikuwa mstari wa mbele tukiona kila kilichoendela,watu 115 walipoteza maisha , kikubwa tuwe watulivu na kuwaombea dua ndugu zetu "Amesema DC Msulwa.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.