WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA HATUA ZA KUJIZUIA NA MAAFA YA MOTO.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akisoma taarifa fupi ya Kumbukumbu ya Wahanga wa ajali ya Moto Msamvu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wa kumbukizi hizo.
Ndugu, Jamaa na marafiki wakizuru makaburi ya Kola leo wakati wa kumbukumbu ya mwaka mmoja wa wahanga wa ajali ya Moto Msamvu.Ndugu, Jamaa na marafiki waliojitokeza makaburi ya Kola leo Agosti 10,2020 , wakati wa kumbukumbu ya mwaka mmoja wa wahanga wa ajali ya Moto Msamvu.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka Wananchi kuchukua hatua za haraka za kuzuia na kupambana na Majanga ya Moto pindi yanapotokea katika maeoeno yanayowazunguka.
Kauli hiyo ,ameitoa leo Agosti 10,2020 katika Makaburi ya Kola yaliyopo Kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro wakati wa kumbukizi za Wananchi walifariki dunia kwa ajali ya Moto Msamvu.
Lukuba, amesema ifike wakati Wananchi waweke tahadhari wenyewe kabla ya kutegemea Jeshi la Polisi au Zima Moto.
Akitoa taarifa fupi ya Kumbukumbu ya Wahanga wa ajali ya moto iliyotokea tarehe 10,8,2019 mwaka jana, amesema kuwa baada ya kutokea ajali ,Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali , Taasisi binafsi na Wananchi walijitokeza kutoa michango mbalimbali ikiwemo ya vifaa na fedha .
Amesema fedha zilizochangwa hadi kufikia tarehe 28,02,2020 zilikuwa ni kiasi cha Shilingi milioni 59,473,000.00 ambapo Ofisi ya Mkoa wa Morogoro ilifungua Akaunti ya benki yenye namba 24910000541 katika Benki ya NMB kwa ajili ya kuhifadhi fedha hizo.
Hata hivyo amesema jumla ya fedha zilizotumika kwa ajili ya ujenzi wa Makaburi hayo ni shilingi milioni 18,ambapo gharama hizo ni pamoja na ujenzi wa Makaburi, Uzio na Mnara wenye majina ya Wahanga wa ajali ya Moto ambapo watatenga tena shilingi milioni 10nkwa ajili ya kumalizia ujenzi uliobakia kama agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alivyoelekeza.
“”Tarehe ya leo mwaka 1 uliopita haitoweza kusahaulika kirahisi kwenye mioyo ya Watanzania kwa kupoteza ndugu zetu katika ajali mbaya ya Moto, Serikali inaungana na ndugu wa Wahanga wote kutoa pole katika siku hii muhimu ya kuwakumbuka ndugu zetu waliopoteza maisha katika janga hili,hakika kila mtu aombe kwa nafasi yake kwani huu ni Msiba mkubwa ambapo kila mmoja kwa namna yake aliguswa na Msiba huu ambao uliyagharimu Maisha ya Mamia ya Wapendwa wetu, kwa niaba ya Uongozi wa Manispaa ya Morogoro tunawashukuru watu wote waliojitokeza kuja kuungana nasi katika siku hii muhimu ya kumbukumbu ya Wahanga wa ajali ya Moto”Amesema Lukuba.
Ikumbukwe kuwa tarehe 10,8,2019 Taifa lilipatwa na tukio la ajali ya Moto uliosababishwa na kulipuka kwa garo la mafuta lililopata ajali eneo la Msamvu kandokando ya barabara ya Morogoro –Dar Es Salaam ndani ya Manispaa ya Morogoro ambapo katika ajili hiyo jumla ya watu 115 walipoteza maisha kati ya hao wanaume walikuwa 109 na wananwake 6.
Lakini ndugu 39 walifanikiwa kuchukua miili ya wapendwa wao na kwenda kuizika maeneo mbalimbali ya nja ya makaburi ya pamoja , huku jumla majeruhi 21 ambao wanaume 16 na Wanawake 5ambapo kwa sasa wanaendeleo vizuri.
“MWENYEZI MUNGU AENDELEE KUWAPA PUMZIKO LA MILELE WAPENDWA WETU, NA TUENDELEE KUWAOMBEA WAPUMZIKE KWA AMANI”.
Post a Comment