MSIMAMIZI WA JIMBO LA UCHAGUZI MOROGORO MJINI ATAKA ZOEZI LA UCHAGUZI LIZINGATIE SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA UCHAGUZI.
Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata Manispaa ya Morogoro wakiwa katika semina ya ufungaji wa mafunzo katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata katika ufungaji wa semina ya mafunzo katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro.
MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka na kuwasisitiza Wasimamizi Wasaidizi Ngazi ya Kata kuendelea kusoma Sheria za Uchaguzi , Kanuni na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza shughuli za Uchaguzi.
Hayo aliyasema hivi karibuni katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro wakati wa kufunga mafunzo ya siku 3 yaliyoanza Agosti 07-09 , 2020 kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi Ngazi ya Kata Jimbo la Morogoro Mjini.
Lukuba, alisema pamoja na kwamba uzoefu ni nyenzo muhimu
katika kufanikisha Uchaguzi lakini pia uzoefu unaweza kuwaponza kwa kufikiri
kuwa wanajua kila kitu na kusahau kujisomea.
“Napenda kuwashukuru wote kwa ushirikiano mlioutoa wakati wa mafunzo
mpaka tumemaliza kwa mafanikio,naamini malengo yaliyokusudiwa yamefikiwa,
lakini lazima mtambue kuwa Tume imewaamini na kuwateua kuwa Wasimamizi
Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ikiwa na imani kuwa kazi hiyo mtaifanya kwa
ufanisi ili kuwezesha Uchaguzi huu kufanyika kwa mafanikio makubwa, nipende
kuwatakia safari njema ya kurejea katika maeneo na kila la kheri katika
utekelezaji wa majukumu yenu ya Uchaguzi””
Aidha, amewapongeza Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata kwa
michango waliyotoa wakati wote wa majadiliano na uzoefu waliobadilishana katika
mafunzo hayo hku akisema maswali waliyojiuliza yalitoa mwanga na uelewa wa
pamoja wa namna shughuli za uchaguzi zinavyoweza kuboreshwa wakati wote.
Mwisho ametoa wito kwa Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata kuendelea
kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na Wataalamu wa afya kuhusu kujikinga na
maambukizi dhidi ya Ugonjwa wa Corona (COVID-190.
Post a Comment