Header Ads

Dc Mjema asema miradi yote ipo salama.







MKUU wa  Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amesema miradi yote ikiwamo ya kimkakati inaendelea vizuri. 


Hayo ameyasema leo  wakati akikabidhi ripoti juu ya miradi ya Ilala kwa Mkuu Wa Mkoa Dar Es Salaam, Mh Paul Makonda wakati Wa kikao cha kusoma ripoti kwa watendaji wote  Wa Mkoa kilichofanyika Ukumbi Wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam Septemba 25/2019. 

Akizungumza hayo, DC Mjema amesema upande Wa Soko la  Kisutu ujenzi unaendelea hadi  kufikia Desemba Mwaka huu wanatarajia kupokea miradi huo wenye thamani ya Bilioni 17 ambapo Manispaa imetenga Bilioni 4 na Bilioni 16 kutoka Kwa Mh Rais Dkt John Magufuli. 

Pia amesema Soko  la  Ilala tayari pesa za ndani Halmashauri imetenga Milioni 74 na zoezi linaloendelea ni  kumtafuta mzabuni.

" Ipo  miradi mingi Hosteli Jangwani, Machinjio Vingunguti, Hospitality Kivule yote ifikapo desemba tunaimani tutakuwa tumekamilisha Ilani ya CCM" Amesema DC Mjema.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.