Header Ads

DC Mjema awabana mbavu TANESCO.





MKUU Wa Wilaya Ilala, Mh Sophia Mjema amewataka TANESCO kupunguza muda walioweka katika kuwapatia huduma wananchi Wa Mbondole Kata ya Msongola.

 Akizungumza na waandishi Wa Habari leo Septemba 26/2019 akiwa katika muendelezo Wa ziara yake  katika Kata ya Msongola, amesema muda waliopanga TANESCO ni mkubwa hivyo ameagiza mpaka kufikia Novemba mwaka huu umeme uwe  umeshafika.

Amesema miradi yote iliyotajwa na TANESCO Ilala, ni ahadi ambazo bado zinawatesa wananchi hivyo ifikapo Novemba Shule ya Msingi Mbondole pamoja na Zahanati zote ziwe zimepata Umeme ili wananchi waone Serikali yao ikiahidi inafanya kazi.

" Haiwezekani kila tukija tunaahidi mambo ya muda mrefu, Rais wetu Dkt John Magufuli ni mtu  Wa vitendo akiahidi anafanya, sasa mnakwama wapi? hiyo bajeti yenu ipunguzeni nataka nikirudi tena hapa nikute umeme umeingia" Amesema Mjema.

Katika hatua nyingine amepiga marufuku michango ya Tuisheni kwa wanafunzi huku akimtaka Afisa Elimu kulichunguza hilo.

   Aidha, amewataka wale wote  walioshindwa kulipa fidia katika kesi ya ardhi  dhidi ya Ndugu Sufini Mbwambo aliyeshinda kesi hiyo Mahakamani kulipa Mara moja kwani wasipofanya hivyo wale waliolipa na kumaliza watazungurushiwa  uzio wao na wasiolipa nyumba zao zitabomolewa.

Amesema wapo waliomaliza fidia 617, waliolipunguza fidia 413 pamoja na wasiolipa 581.

" Hivi nyie msiolipa mnataka nilipe Mimi? niliwaonea huruma  kesi ile tukakubaliana maana penginevyo kuna watu tungelikuwa tumeshawazika na wengine wangepata kiharusi sasa nawaomba mlipe la  sivyo namruhusu aliyeshinda kesi kubomoa nyumba zenu" Ameongeza kusema DC Mjema.

Pia amekagua madarasa mapya 4 shule ya Sekondari Mbondole yenye thamani ya Milioni 70.

Hata hivyo katika kutatua kero ya usafiri ameagiza SUMATRA kuangalia utaratibu Wa kuweka Ruti  itakayo unganisha usafiri Wa mijini ili kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi Wa Mbondole.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.