DC Mjema amtumbua Kiongozi kwa ufisadi.
MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema amemtumbua Kiongozi Wa Soko la Zingiziwa kwa madai ya kuhusika na rushwa katika ugawaji wa Vizimba.
Tukio hilo limetokea leo kata ya Zingiziwa wakati Wa muendelezo Wa Ziara yake ya kutatua kero za wananchi Wilani kwake.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari, amesema Kiongozi Huyo anayejulikana kwa jina la Hussein Mgalusi anae husika na ugawaji Wa vizimba amekuwa katika kashfa ya rushwa wakati Wa ugawaji vimba hivyo.
Aidha ameutaka Uongozi Wa Soko kuhakikisha wanawahudumia wananchi wao bila ya upendeleo wala chembe chembe za rushwa.
" Hili ni fundisho na yule mwenye Tabia kama hizi tutamshughulikia hivyo Mzee Mgalusi tumemuondoa tunaendelea na upelelezi tukibaini basi pesa zote zitarudishwa na kumchukulia hatua Kali zaidi" Amesema DC Mjema.
Mpaka sasa jumla ya wafanyabiashara 680 washapatiwa vizimba kati ya Vizimba 800 vinavyotakiwa kugaiwa. Aidha uongozi huo Wa Soko umetenga vizimba hivyo katika biashara tofauti kama vile, Vizimba vya Mali mbichi 288, Vizimba vya duka 320, Vizimba vya nguo 96 pamoja na Vizimba vya Mama na Baba lishe 96.
Naye Mwenyekiti Wa Kamati ya Soko hilo, Ndugu Hassan Namkwacha, amesema licha ya vizimba, lakini wanajenga fremu za duka kwa kila fremu inagharimu shilingi laki 3 na nusu (35,000/=) pesa za ujenzi nje ya vifaa na ujenzi Wa banda unachukua shilingi Elfu 25.
"Bado tupo katika utaratibu Wa kuwaongeza wafanya biashara hivyo maagizo ya DC wetu tunayachukua na kuyafanyia kazi ili kuleta utulivu na Amani kwa wafanya biashara" Amesema Kiongozi huyo.
Katika hatua nyinge DC Mjema ameutaka uongozi Wa SUMATRA kushirikiana na wafanyabiashara kuhakikisha zinapatikana bara bara zitakazo unganisha usafiri Posta , Kariakoo hadi Zingiziwa.
Post a Comment