RC MAKONDA AWAAGIZA WAKUU WA WILAYA KUHAKIKISHA UGAWAJI WA VITAMBULISHO VILIVYOTOLEWA NA RAIS MAGUFULI VINAMALIZIKA KABLA YA MWEZI MACHI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* amewaagiza wakuu wa Wilaya kuhakikisha hadi kufikia *01/03/2019* kila mfanyabiashara mdogomdogo anakuwa na *Kitambulisho cha utambuzi* kilichotolewa Na *Rais Dkt. John Magufuli* huku akiwataka wafanyabiashara *kuchangamkia fursa* hiyo.
*RC Makonda* amesema kuwa baada ya Tar *01/03/2019* mfanyabiashara yoyote atakaekutwa hana *kitambulisho, leseni ya manispaa* au vielelezo vya kukipa kodi *TRA* atajikuta *mikononi mwa vyombo vya dola* kama muhujumu Uchumi.
*Mhe. Makonda* ameyaeleza hayo leo wakati wa *kikao na watendaji wote wa mkoa* kilichoenda sambamba na *kugawa vitambulisho* vya wafanyabiashara wadogowadogo kwa *Wakuu wa Wilaya* na kufanya mkoa huo kuwa *kinara* kwa kupokea takribani *vitambulisho 175,0000* kutoka kwa *Rais Magufuli.*
Aidha *RC Makonda* amesema baada ya *01/03/2019* serikali ya mkoa itawaingiza wafanyabiashara hao katika *mfumo wa kisasa* (Database) utakaowezesha serikali kuwafikia na kuwapa *mafunzo ya namna kukuza biashara zao* ili mwisho wa siku wafikie *uchumi wa Kati.*
Pamoja na hayo *RC Makonda* amewatahadharisha watendaji *wanaowatoza kiasi kikubwa cha fedha* ya kitambulisho tofauti na *bei elekezi ya Tsh 20,000* huku akiwahimiza wafanyabiashara *kuchangamkia fursa hiyo waliyopewa na Rais.*
Mbali na Vitambulisho *RC Makonda* ametoa miezi miwili kwa *Wakurugenzi wa Manispaa* kuhakikisha *Leseni za wafanyabiashara zinaingizwa katika mfumo mmoja* ikiwa ni pamoja na *kuharakisha utoaji wa leseni* ili kupunguza *usumbufu* kwa wananchi.
Post a Comment