Header Ads

DC Mjema awatuliza Wavuvi wa Samaki Feri.










MKUU wa  Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, Leo Jumanne Januari  29 mwaka 2019 ametembelea Soko la  Samaki Feri baada ya Wavuvi hao  kuketa mgomo.

 DC Mjema amewaeleza Wavuvi hao  kuwa Waziri wa  Mifugo na Uvuvi , Mh Luhaga Mpina Leo mchana atafika eneo hilo  kwa ajili ya kuzungumza nao.

Jana Fungamano la  Vyama Vya Sekta ya Uvuvi Ukanda Wa pwani ya Tanzania lilitangaza Wanachama wake kusitisha shughuli za Uvuvi kwa madai ya mwenzao mmoja kuuwawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa na kumuomba Mh Rais John Magufuli kuingilia kati.

Mbali na kuwatembelea Wavuvi hao , amepata nafasi ya kusikiliza kero zao na kuwataka waendelee na kazi kwani Serikali yao sikivu na imewasikia.

" Nimesikia kero zenu, lakini sitazungumza chochote kwa sasa, tumsubiri Waziri wetu yuko njiani akitokea Dodoma anakuja kuwasikiliza" Amesema.

Ikumbukwe kwamba vugu vugu hilo la  migomo limetokana baada ya Wavuvi kusitisha shughuli za Uvuvi kutokana na kukamatwa wakidaiwa kutumia nyavu zisizo rasmi
.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.