Header Ads

DC Mjema atoa agizo kwa Afisa Elimu Sekondari kutoa taarifa za kina kwa wanafunzi 6000 walioshindwa kuripoti Shuleni.






















MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, ametoa miezi 3 kwa Afisa Elimu Sekondari kuhakikisha anapatiwa taarifa za kina juu ya wanafunzi 6000 kutohudhuria Shuleni tangia matokeo ya ufaulu wao  yalivyotoka.

Hayo ameyasema Leo Mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea baadhi ya shule mpya za Sekondari zilizopo Wilaya ya Ilala pamoja na Shule zilizopo katika uongezwaji wa  Madarsa mapya na ukarabati.

 Akizungumza na Waandishi wa  Habari Leo, DC Mjema, amesema kuwa mpaka sasa ni jumla ya Wanafunzi 15126 sawa na 70% wameshawasili Shuleni ambapo Wanafunzi 6274 hawajahudhuria sawa na 29.3%.

Licha ya hapo, amesema ni Wanafunzi 26 tu ambao taarifa zao nu kwamba wamehamishiwa Shule binafsi na Wanafunzi 127 wamehamia Mikoani kutoka na hama hama za wazazi wao, hivyo kufanya Wanafunzi 153 kuwa na taarifa.

 Kufuatia wingi huo Wa idadi ya Wanafunzi wasioripoti DC Mjema, ametoa miezi 3 taarifa zao ziwe zimenfikia ili hata kama kuna  wazazi wamewaozesha watoto zao hatua Kali za kisheria zitafuatwa.

Amesema kuwa katika kuona zoezi hilo linafanikiwa, amemuagiza Afisa Elimu Sekondari kuhakikisha wanatengeneza kamati ndogo ya kujua sababu za Wanafunzi hao kishindwa kuhudhuria Shuleni.

 " Kwanza niwapongeze waalimu kwa kuwapokea Wanafunzi wetu, kwani idadi hii kubwa ya ufaulu imetokana na jitihada za Uongozi Wa awamu ya tano  chini ya Rais wetu mpendwa Mh: John Magufuli ya Elimu bure, pia nakuagiza Afisa Elimu Sekondari tengenezeni kamati ndogo ili kubaini ni kwanini Wanafunzi Hawa 6000 hawajahudhuria Shuleni baada ya hapo muje na taarifa za kina mezani kwangu tuweze kuona tunafanyaje lengo ni kila mwanafunzi asome  na hatutaki kuona katika Wilaya yangu kuna  Wanafunzi wamefaulu kisha hawasomi kwani Serikali inajitahidi sana licha ya kuwepo na changamoto" Amesema DC Mjema.

 Pia DC Mjema ametembelea Shule ya Sekondari Kasulu na kukuta ujenzi ukiendelea hivyo katika ujenzi huo amehakikishiwa ifikapo tarehe 25 mwezi Februari, 2019 watakuwa wameshakabidhi majengo hayo na wapo katika mpango Wa kujenga madarasa ya ghorofa kutokana na ufinyu Wa ardhi na tayari jumla ya Shilingi Milioni 250 washaingiziwa kwenye akaunti yao tayari kwa utekelezaji.

Mbali na Shule ya Kasulu amepata nafasi ya kutembelea Shule ya Sekondari ya Buguruni Moto ambapo changamoto kubwa ni uhaba Wa Waalimu wa Masomo ya Hisabati pamoja na fiziksi na vitendea kazi  kama vile vitabu hawana kabisa.

Aidha katika kutatua changamoto hizo zinazo ikabili Shule hiyo pamoja na Shule ya Msingi buguruni Ghana ameahidi kuwasaidia ili wanafunzi wasome vizuri na kuwapata wanasayansi wengi katika kuelekea uchumi Wa kati.

Pia katika ziara hiyo amemalizia katika Shule ya Sekondari Kinyamwezi huku akiahidi kuzifanyia kazi  changamoto zao zikiwemo za Elimu na waalimu kwa ujumla katika kuwasaidia wale waliopandishwa madaraja na mishahara yao haijapanda.

Katika ziara hiyo, hakuacha mbali huduma za Afya kwani ametembelea Kituo cha Afya cha Mnyamani na kukuta hatua zote muhimu zimekamilika kinachosubiriwa ni kufunga vifaa tu.

Pia hakuondoka hivi hivi, amepanda mti ikiwa ni kumbu kumbu yake  katika hospitali  hiyo.
bu yake  katika hospitali  hiyo.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.