DC Mjema amtolea uvivu Kiongozi Wa Wamachinga Gongolamboto.
MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amemuagiza OCD Wa Ukonga kumkamata Mwenyekiti Wa Wamachinga Gongolamboto, Christopher Kidiga, baada ya kulalamikiwa kuwatoza Shilingi elfu 10 Wamachinga ili kuwapatia fomu za kuchukua vitambulisho vya Biashara.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari, DC Mjema, amesema Mwenyekiti huyo ameenda kinyume na maagizo ya Mh : Rais John Magufuli ya kuwataka Wajasiriamali kuwa na vitambulisho kwa utaratibu maalumu..
DC Mjema amesema Vitambulisho hivyo havijatolewa kwa ajili ya kuwanufaisha watu wengine Bali kwa Wanyonge na wajasiriamali wadogo wadogo huku wakitakiwa kulipa Shilingi elfu 20 tu.
" Lazima msome alama za nyakati , sio kila kitu kwenu ni fursa hill ni agizo la Rais wetu Dr John Magufuli la kuwataka Wamachinga, Mama ntilie na Wajasiriamali wadogo wadogo kuwasaidia kufanya shughuli zao bila buguzi sasa mnavyokuja na tozo zenu lazima tuwachukulie hatua, hili ni fundisho kama wapo wengine pia tutawashughulikia" Amesema DC Mjema.
Amesema ili upate vitambulisho unatakiwa uwe na faida ya mwaka isiyopungua milioni 4 sasa mtu akizidi hapo TRA watadili nae.
Amewataka wale wote wenye sifa hizo waende Ofisi ya Kata kwa Mtendaji wakiwa na majina kamili, mtaji wake Wa Biashara, anapoishi, na mawasiliano yake akiambatanisha na fomu yenye Barua na picha pamoja na 20000 atapatiwa huduma na sio kutapeliwa.
Pia amewataka wale wote watakao ombwa rushwa watoe taarifa mapema kwa Ma Afisa Tarafa wake.
Post a Comment