Header Ads

MPANJU APONGEZA WANANCHI WA KIEGEA 'A' MANISPAA YA MOROGORO KUANZA UJENZI WA KITUO CHA POLISI

NAIBU  Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju, amewapogeza Wananchi wa Mtaa Kiegea ‘A’  Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro kwa maamuzi ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Polisi kwa kutumia nguvu kazi za Wananchi na michango yao.

Pongezi hizo amezitoa wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Machi 31-2026 akiambatana na Viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa wa Morogoro na Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mapokezi hayo, Mpanju,  amewahamasisha kumalizia ujenzi wa kituo hicho kwa wakati ili kiweze kuwahudumia pamoja na wananchi maeneo jirani ikiwemo Kata tatu Lukobe, Mkundi na Kihonda.

Aidha, Mpanju, ametoa jumla ya mifuko 45 ya saruji, huku akiwataka wadau mbalimbali waendelee kuchangia na wizara yake itahakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Desemba 2026 na kuona ndoto ya wananchi wa Kiegea ya kuwa na Kituo cha Polisi kwa ajili ya usalama na ulinzi  wa mali zao unakamilika.

Mpanju, mbali na kukagua ujenzi huo, pia amekuatana na makundi mbalimbali katika Ukumbi wa Kapinga Mkundi  ikiwemo Kundi la Wanawake, Vijana na watu  wenye ulemavu kwa ajili ya kuwaelezea fursa zinazotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii.

Miongoni mwa fursa alizozitaja ni fursa ya mikopo ya asilimia 10 ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu, fursa ya zabuni za serikali ya asilimia 30 kwa makundi maalum , fursa ya mikopo kuendeleza wafanyabaishara ndondogo maarufu machinga pamoja na fursa zinazotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Vijana ya bilioni 200 kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Naye Meya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Khalid Matengo, amewapongeza wananchi kwa hatua walichukua kwani usalama wa wananchi unaanza na wao wenyewe.

Matengo,amesema kuwa katikakuona ujenzi huo unafanikiwa Ofisi ya Meya itachangia jumla ya matofali 2000 ili kuwaunga mkono wananchi wa Kiegea kifanikisha ujenzi huo.

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro , Christopher Komba, amesema Manispaa ya Morogoro katika ujenzi wa Kituo hicho umesaidia vifusi na kutoa gari kwa ajili ya ubebaji wa vifaa lakini bado inaendelea kuona nguvu ya kuongeza ili ujezi huo ukamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Diwani wa Kata ya Kihonda, Eng. Mhe. Ramadhani Myolele, amesema mradi huo umeibuliwa na wananchi mara baada ya kuona changamoto za kiuharifu na kuanza kucnagia fedha na kutoa nguvu kazi.

Eng. Myolele ,amesema kuwa , mradi huo una malengo ya kusogeza huduma za kipolisi karibu na Wananchi pamoja na kujenga mahusiano mazuri kati ya Polisi na Wananchi.

Kwa upande wake, wa Mtaa wa Kiegea ‘A’ Ezekiel Songa, amewapongeza wananchi kwa kutoa nguvu kazi na kuchangia fedha za kuanza kwa Kituo hicho huku akisema  ili Polisi wafanye kazi kwa uadilifu wanatakiwa kuwa na mazingira bora ya kufanyia kazi, hivyo kituo hicho kitakapo kamilika kitakuwa msaada kwa wananchi wa Mtaa wa Kiegea ‘A’ ,Kata ya Kihonda na Kata jirani ikiwemo Lukobe, Mkundi pamoja na Katab ya Kihonda

Mkazi wa Kiegea ‘A’ Undule Anthony, amesema walikuwa wanateseka kufuata huduma ya Polisi wanasafiri umbali mrefu kwa kutumia gharama ya shilingi 5,000/= hivyo kumalizika kwa mradi huo kutawapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu na kupunguza vitendo vya uharifu katika Mtaa wa Kiegea.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.