Header Ads

KAMATI YA SIASA CCM KATA YA MJI MPYA WAKOSHWA NA UTENDAJI WA UONGOZI WA KATA YA MJI MPYA CHINI YA MHE. MSELEMA ,YAAHIDI KUIPA USHIRIKIANO



KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi  Kata ya Mji Mpya   imepongeza Uongozi wa Kata ya Mji Mpya ukiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Iddi Mselema  katika kuleta maendeleo kwa Wananchi wa wa Kata hiyo pamoja na utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mji Mpya , Ndug. Kombo Mkumilwa kwa niaba ya ya wajumbe wa Kamati hiyo  , katika ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwenye Kata ya Mji Mpya Machi 25-2026.

Mkumilwa, amesema Uongozi wa Kata ukiongozwa na Diwani umeonesha uzalendo katika kuhakikisha ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025 hadi 2030 , inatekelezwa kwa vitendo kwa kutumia makusanyo yao ya ndani, Fedha kutoka Serikli kuu pamoja na Fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo.

‘” Tunaupongeza Uongozi wetu wa Kata ukiongozwa na Mhe. Mselema, kwa kweli wamezitendea haki fedha za miradi, na kuitendea   haki ilani ya uchaguzi  ya CCM ya mwaka 2025-2030 , Kata yetu ni mfano wa kuigwa kwa haya yaliyofanyika ni alama tosha na taswira nzuri inayoonekana kwa Wananchi, tumeshuhudia ujenzi wa madarasa ya kisasa Shule ya Msingi Mwembesongo, huduma bora zinazotolewa kwenye Zahanati yetu hususani huduma ya kujifungua na ile ya meno, barabara ya zege yenye ubora wa hali ya juu, daraja la Fungafunga na mengine yote yanaashiria Utawala bora ,  tunaamini yapo mengi yanakuja kwetu kikubwa tuendelee  kumpa ushirikiano Diwani wetu na ametuahidi kufuatilia kwa karibu kipande cha barabara kilichobakia kilichoishia Kituo cha Polisi kukamilika ili kuondoa adha ya watumiaji kipimndi cha mvua na daraja letu la fungafunga kukamilika  hili ni jambo jema litakalowasaidia Wanafunzi na wananchi kupata urahisi wa usafiri tunajivunia kuwa na Kiongozi mchapakazi kama huyu Mhe. Mselema " Amesema Mkumilwa.

Naye Diwani wa Kata ya Mji Mpya, Mhe. Iddi Mselema, amesema ataendelea kushirikiana na wananchi ili kukamilisha miradi ya maendeleo  huku akiihakikishia Kamati ya Siasa  Utawala bora hususani katika  thamani halisi ya fedha inaonekana  Katika miradi hiyo kwani mbali na kutumia fedha za ndani, Serikali kuu na wadau, lakini pia  kiasi kinachotumika katika ukamilishaji wake vinaenda sambamba na ubora .

Miongoni mwa miradi ambayo Kamati ya Siasa imetembelea ni Zahanati ya Kata ya Mji Mpya, Shule ya Msingi Mwembesongo, Shule ya Msingi Kaloleni, Eneo la ujenzi wa Daraja la Funga Funga, Barabara ya zege pamoja na Soko la Mji Mpya.




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.