WAFANYABIASHARA VINGUNGUTI WAONYESHWA KUGUSWA NA JUHUDI ZA MEYA KUMBILAMOTO KINAMAMA WAMEAMUA KUVUA KANGA NA VITENGE ILI KUMTANDIA APITE
Wafanyabiashara wa Nyamachoma pamoja na baba na mamalishe wa eneo la Vingunguti, jijini Dar es Salaam, wameonyesha kuguswa na kupongeza juhudi za Diwani wa Kata ya Vingunguti ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Omary Kumbilamoto, kwa namna anavyowapigania kuhakikisha wanafanya biashara katika mazingira bora, salama na ya kisasa.
Hayo yamejili Mei 19-2025 , kwenye kikao Maalum cha wafanyabiashara hao mara baada ya kukamilika kwa soko la Kisasa la Nyamachoma ambalo limejengwa kwa zaidi ya shilingi milioni 700 ambapo uzinduzi wake unatarajiwa kufanyika mwishoni wa wiki hii.
Kumbilamoto , amesema lengo la Serikali ya Jiji la Dar Es Salaam ni kuboresha maeneo ya masoko pamoja na wafanyabiashara wake ikiwa ni mpango mkakati wa kuboresha masoko yote ya ndani ili kuiwezesha miradi hiyo kuwaingizia kipato cha mtu mmoja mmoja na Jiji na Wakazi wa Vingunguti kwa ujumla.
Aidha,Kumbilamoto amesema kuwa kuboreshwa masoko ya ndani yatachangia ongezeko la pato la Halmashauri ya Jiji kama ilivyo kwa miradi mingine mikubwa ikiwamo wa Soko Kuu pamoja na vitega uchumi vyengine.
Hata hivyo,Kumbilamoto amempongeza Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anazozifanya katika kuboresha miundombinu ya biashara hususani kwa Wajasiriamali wadogowadogo maarufu kama Wamachinga.
Post a Comment