Header Ads

DIWANI KIHANGA AWASILISHA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM ILIYOSHEHENI MAZURI KATA YA MAZIMBU, AWAAHIDI KUENDELEA KUWAPA USHIRIKIANO



DIWANI wa Kata ya Mazimbu na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka 4 na nusu akiwa madarakani katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Kata ya Mazimbu.

Mkutano huo umefanyika Katika Ukumbi wa Atubela Kata ya Mazimbu Mei 25-2025.

Akizungumza na wajumbe kwenye Mkutano huo, amesema pamoja utekelezaji wa miradi lukuki katika Sekta za Afya, Maji, Miundombinu na Elimu,likini ameendelea kukuza mahusiano bora baina ya Uongozi wa CCM na Serikali kupitia Ofisi ya Kata na Ofisi ya Manispaa ya Morogoro.

Kihanga,amesema kuwa Katika kuboresha Elimu ya awali kwa shule za Msingi, ameboresha miundombinu ya madarasa  pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo.

Aidha,amesema wakati anaingia madarakani, kulikuwa na changamoto ya upungufu wa vifaa vya kufundishia lakini katika kipindi chake cha miaka 4 na nusu changamoto hizo kwa sasa hakuna ambapo juhudi hizo zimetokana na uhamasishaji wake , pamoja na nguvu ya Ofisi ya Manispaa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Amesema upande wa shule ya Msingi Mzimbu A  kwa  upande wa Taaluma imekuwa ikishika nafasi ya 9 mfululizo kwa Shule za Msingi za Manispaa ya Morogoro.

Aidha, katika kipindi cha miaka 4 na nusu ya Uongozi wake, amechangia kwa kiasi kikubwa  taaluma za shule za Mazimbu pamoja na kuchangia milioni 1 kununua madawati shule ya Msingi Mazimbu A.

Mbali na ununuzi wa madawati lakini amechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa madarasa 5 Shule ya Msingi Mazimbu A pamoja na kuhamasisha wananchi kuchangia katika ujenzi wa madarasa hayo.

Kwenye  shule ya Msingi Mazimbu B ,amechangia kiasi cha shilingi  laki 6 , tofaili 250 na mifuko 6 ya saruji katika kufanikisha ujenzi wa matundu 24 ya vyoo katika shule hiyo.

Pia upande wa madarasa ,Mhe. Kihanga,amesema amechangia kiasi cha shilingi laki 6 na matofali 300 katika kufanikisha ujenzi wa madarasa 4 katika shule hiyo.

Pia katika kuona wanafunzi wenye mahitaji maalum wanasoma katika mazingira rafiki,amehakikisha ujenzi wa darasa 1 shule ya Msingi Mazimbu A linajengwa .

Mhe. Kihanga,amesema shule ya Maizmbu A na B zilikuwa na changamoto ya maji hivyo alianza kulipia madeni ya bili za shule hizo pamoja na kutafuta wafadhili ambao ni EGG Tanzania waliofanikisha  uchimbaji wa visima katika shule hizo huku shule ya Msingi Mazimbu A akinunua  tenki lenye ujazo wa lita 3000 na Mazimbu B kununua  tenki lenye ujazo wa lita 5000

Katika sula la motisha kwa walimu na wanafunzi,Mhe. Kihanga amesema inapofikia mitihani ya Taifa amekuwa na utamaduni wa kuwasalimia wanafunzi na kuwatia moyo pamoja na kuwamotisha walimu mara baada ya matokeo kwa kuwapa kiasi cha fedha cha shilingi laki 5 kwa kila shule ili kuongeza kasi ya ufundishaji kwa walimu wa shule hizo.

Mhe.Kihanga,amesema licha ya kuwamotisha walimu kifedha lakini amekuwa akijitolea fedha kwa ajili ya kuandaa mitihani ya kujipima kwa wanafunzi wanapokaribia kufanya mitihani ya Taifa.

Kwa upande wa shule ya Sekondari Mazimbu, Mhe. Kihanga amesema awali hakukuwa na shule Kata hiyo lakini kwa sasa Kata ina shule ya Sekondari ambapo katika jitihada zake kwa kushirikiana na nguvu ya wananchi na mchango wa fedha kutoka Manispaa na Serikali Kuu  wamefanikisha ujenzi wa shule hiyo.

Aidha, Shule ya Sekondari Mazimbu ina jumla ya madarasa 31 ambapo madarasa 13 yametokana na nguvu za wananchi na mchango wa Mhe. kihanga.

Aidha,Mhe. Kihanga,amempongeza Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abood kwa jitihada zake za kuipatia shule ya Sekondari Mazimbu  viti 310 na meza 310 pamoja na jitihada za Mkurugenzi wa Manispaa ya kutoa viti 50 na meza 50 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.

Mhe. Kihanga,amesema katika upande wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, amesema vikundi 13 vimenufaika na mikopo hiyo huku akiwataka Vijana, Wanawake na Walemavu kuendelea kuunda vikundi kwa ajili ya kupata fedha hizo.

Pia, Kihanga,amesema ameboresha sana miundombinu ya barabara katika Kata hiyo mfano wa barabara korofi ya Barakuda , barabara ya kuingilia kwa Afande Sele , kipande cha barabara ya kwenda SUA Ndani zote zilikuwa ni changamoto na sasa  zinapitika vizuri na kiunganishi kwa wananchi.

Pia, kihanga,amesema mpango uliopo kwa sasa ni kuhakikisha barabara inayotokea Ipoipo kuwe na daladala zinazounganisha barabara hiyo kwenda Msamvu kupitia barabara ya MUM pamoja na Barabara ya FK ipite magari kwenda St.Anna.

Katika upande wa Afya, Kihanga amesema Kata hiyo haikuwa na uduma za Afya lakini kwa sasa kuna Zahanati kubwa na inaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Pia ,Mhe. Kihanga,amesema katika kuona Kata hiyo inaendelea kuwa na amani,  tayari ameshaanzisha ujenzi wa Kituo cha Polisi ambacho anatarajia muda sio mrefu Kitaanza kutoa huduma na kuifanya Kata hiyo kuimarisha ulinzi na usalama.

Katika suala la utawala bora, Mhe. Kihanga,amesema ameimarisha Utawala bora kwa watumishi wa Kata hiyo lakini pia kuimarisha maeneo ya utendaji wa Kazi kwa kukarabati Ofisi ya Kata mabapo bado ukarabati unaendelea ili watumishi wa Kata hiyo kufanya kazi katika mazingira rafiki.



Kwa upande wa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini ambaye ndiye mgeni rasmi ,Ndg. Maulid Chambilila, amesema ameridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM chini ya Diwani wa Kata hiyo kwani imejitosheleza na imebeba matumaini ya wananchi wa Kata ya Mazimbu.

Chambilila,amewataka Viongozi wa Kata hiyo kuendelea kumpa ushirikiano Diwani wao kwani bado yupo madarakani  ili atimize wajibu wake ya kuwatumikia wananchi wake.

Aidha, Chambilila,amesema Uongozi wa Mhe. Kihanga uliotukuka ndio umesababisha Mazimbu kupata maendeleo makubwa katika kipindi chake cha miaka 4 na nusu hivyo waendelee kuwa na imani nae.

" Tunaelekea kwenye uchaguzi, Mzee huyu kafanya mengi sana na mazito, nyie ndio wa kupima ,sisi CCM hatutaki viongozi wa kujaribu tunataka viongozi wa Kazi watakaomsaidia Dkt Samia kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi, shirikianeni na Diwani wenu, muda wa uchaguzi bado, acheni kampeni uchwara za chini chini tutakao wabaini tutawachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu" Amesema Chambilila.

Mwisho Chambilila,amewataka Viongozi wa CCM Kata ya Mazimbu kutembea kifua mbele kwani Ilani ya CCM imetekelezwa kwa ufanisi wa hali ya juu chini ya Mhe. Kihanga kwa kushirikiana na Viongozi wa CCM  na Ofisi yake ya Kata.

Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mazimbu,Ndg. Liberat Njau,  amesema hali ya kisiasa Kata ya Mazimbu inaridhisha kwani CCM imekuwa ikionesha mahusiano mazuri baina ya Matawi ya CCM ,Mabalozi, Wajumbe wa Serikali za Mitaa ,Wenyeviti wa Mitaa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Serikali ya Kata.

Njau,  anampongeza Diwani Kihanga, kwani amekuwa na mchango mkubwa sana katika kuimarisha uhai wa Chama  Chama kwa kuwezesha matofali 1000 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Kata ya CCM.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.