Header Ads

BALOZI BATILDA ATAKA MAONI YA WADAU KUFANYIWA KAZI KUELEKEA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MSHARIKI 2025.


MKUU wa Mkoa wa Tanga na Mwenyekiti wa Kikao Cha Maandalizi ya Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Mashariki, Mhe. Balozi Batilda Burhan ameiagiza kamati ya uratibu wa masuala ya maadhimisho ya wakulima maarufu kama 

Nanenane kuhakikisha wanafanyia kazi mapendekezo, maoni na ushauri wa wajumbe wa Kamati Kuu ambayo ni pamoja na kuhakikisha maonesho ya mwaka huu yanaongeza tija kwa waandaaji na wanufaika na kuepuka kuyafanya kwa mazoea.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, ambaye ndiye mwenyeji wa kikao hicho amesema suala la upatikanaji wa maji toshelevu katika uwanja huo ni la muhimu sana na ameahidi kulishughulikia huku akizitaka halmashauri zote kuhakiksha zinakuwa na vyombo vya kuhifadhia maji.

Kikao hiki ni cha kwanza kwa mwaka 2025 na hukutanisha wajumbe kutoka mikoa minne inayounda Kanda ya Mashariki, ambayo ni Tanga, Pwani, Dar-es-Salaam na Morogoro.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.