Header Ads

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BVR MANISPAA YA MOROGORO WAASWA KUFANYA KAZI KWA UNADHIFU NA HAKI









Maafisa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki waaswa kufuata miongozo na maelekezo ya Tume Huru  ya Taifa ya Uchaguzi ili kufanya kazi kwa unadhifu na haki. 

Hayo yamesemwa wakati wa kufunga mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura yaliyofanyika katika Jengo la Samia Suluhu Hassan Chuo Kikuu cha SUA ,februari 26-2025.

Akizungumza  wakati wa mafunzo hayo,  Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Morogoro Mjini, Faraja Maduhu  amewataka watenda kazi hao kusoma  kwa umakini sheria ya Uchaguzi, kanuni za uboreshaji, maelekezo na miongozo yoye inayotolewa na Tume ili kazi yao  ifanyike kwa unadhifu na haki.

Aidha , Maduhu, amesisitiza juu ya mawasiliano kati ya wataalamu hao na maafisa wa Tume upande wa TEHAMA ili ikiwa kutakuwa na changamoto ipatiwe utatuzi mapema na kuzingatia  muda kwenye kazi sanjari na huduma nzuri kwa wateja wanaokuja kwa ajili ya kujiandikisha.

Mafunzo yamefanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 26 hadi 27 Februari 2025  ambapo jumla ya maafisa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaaa vya BVR 1000 wamepatiwa mafunzo tayari kwa ajili ya kwenda kuanza zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura linalotarajia kuanza Machi 1-2025.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.