DC KILAKALA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI DCC CHA KUJADILI MAPENDEKEZO YA BAJETI YA MWAKA FEDHA 2025/2026 MANISPAA YA MOROGORO
MKUU wa Wilaya ya Morogoro ,Mhe. Mussa Kilakala, ameongoza Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) Manispaa ya Morogoro kikao kilicholenga kujadili mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Manispaa ya Morogoro.
Kikao hicho kilifanyika Januari 31/2025 katika Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo viongozi wa vyama mbalimbali vya Siasa.
Akifungua kikao hicho , DC Kilakala, amesema kuwa kikao hiko kilikuwa na lengo la kujadili mapendekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na kuwaomba wajumbe kupitia vizuri bajeti hiyo kwa maslahi mapana ya Manispaa ya Morogoro na Wilaya kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg.Fikiri Juma, amemshukuru DC Kilakala, huku akimuhakikishia kuwa CCM Wilaya ya Morogoro itaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ili wananchi wafaidi matunda ya Serikali yao.
Wajumbe mbalimbali wamempongeza DC Kilakala, na kuwaomba wataalam waendelee kupanga mipango na Bajeti zinazo akisi moja kwa moja uhalisia kwa maendeleo ya Manispaa ya Morogoro.
Post a Comment