WATAHINIWA 10404 KUFANYA MITIHANI YA KUMALIZA DARASA LA SABA MANISPAA YA MOROGORO
JUMLA ya watahiniwa 10404 wanatarajiwa kufanya mtihani wakumaliza elimu ya msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambao unafanyikanchini kote Septemba11-12 siku ya Jumatano na Alhamisi mwaka 2024.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi na Awali Manispaa ya Morogoro, Fabian Gregory akiwa Ofisini kwake leo Septemba 9-2024.
Gregory amesema kuwa jumla ya shule za msingi 110 zikiwemo Shule za Serikali na Shule binafsi zinatarajia kufanya mitihani hiyo .
Akizungumzia kuhusu maandalizi, amesema maandalizi yanakwenda vizuri na kuwa vituo vya kufanyia mitihani vipo tayari.
Amesema kuwa katika mitihani hiyo, Shule za Serikali ni 72 na shule binafsi 38 huku wanafunzi wa kike wakiwa 5453 na wakiume wakiwa 4951.
“Sisi kama Idara ya Elimu tunaamini tumewaandaa vizuri wanafunzi na wamepata mafunzo kutoka kwa walimu wao hivyo tunatarajiakuwa watafanya vizuri mitihani yao,”Amesema Gregory.
Aidha, Gregory, amewataka wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani hiyo kuwa watulivu na kujibu maswalim inavyopaswa.
Hata hivyo,amesema kuwa mitihani hiyo nisehemu ya kuwapima uelewa wantahiniwa hao katika kipindi cha miaka saba waliyokuwa shuleni na watakao faulu watajiunga na kidato cha kwanza mwakani 2025.
"Naendelea kuwasihi wanafunzi wa darasa la saba kutokuwa na hofu na hivyo wanapokuwa kwenye vyumba vya mitihani wayapitie na kuyasoma vizuri maswali na kuyajibu inavyotakiwa|" Ameongeza Gregory.
Mitihani ya darasa la saba kitaifa inahusishamasomo mbalimbali yakiwemo ya Hisabati, Kiswahili, Kingereza, Maarifa ya Jamiina Sayansi ambayo inatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfulululizo.
Post a Comment