Header Ads

MAAFISA WATENDAJI WA KATA NA MITAA MANISPAA YA MOROGORO WAPATIWA MAFUNZO YA UBORESHAJI KAZI


WATUMISHI wa Manispaa ya Morogoro kada ya watendaji wa Kata na Mitaa  wamepatiwa mafunzo elekezi  yatakayowasaidia katika kuboresha utendaji wao wa kazi  ili kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu  katika maeneo yao ya utendaji kazi.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali watu Manispaa ya Morogoro,,Pilly Kitwana, Septemba 19-2024 kwenye ukumbi wa Manispaa Ofisi Kuu.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Kitwana,amesema amewataka watendaji hao kuzingatia maelekezo yatakayotolewa ili wakayatumie katika kuboresha utendaji kazi wao kwa kuzingatia sheria kanuni na maadili ya kiutumushi.

“Jifunzeni vizuri ili mjue Sheria na Kanuni zinazowaongoza katika utendaji kazi wenu ili msiyumbishwe pale mnaposimamia utekelezaji wa kazi. Ikumbukwe watendaji ndio wasimamizi wa utekelezaji wa kazi na shughuli nyinginezo za maendeleo katika Kata na Mitaa yenu" Amesema Kitwana.

Akiwasilisha mada,Mhadhiri wa Chuo Cha Umma TPSC ,Gasper Kisinza, amefafanua kuwa, utumishi wa Umma unategemea nidhamu kubwa kwa watumishi ili kuepuka migogoro na muajiri itakayopelekea kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Gasper, amesema watumishi wanapaswa kufikia malengo ya kinidhamu ili kudumisha utumishi wenye weledi. Amesisitiza watumishi waepuke makosa makubwa na madogo ya kuitumishi ili kujiepusha na migogoro dhidi ya muajiri na jamii wanayoihudumia.

‘’Watumishi wa tuhakikishe tunazingatia kanuni za utendaji katika utumishi wa umma, ikiwemo kuzingatia masaa ya kazi, mahudhurio sahihi, kuzingatia kanuni na miongozo ya kazi katika jamii tunazoishi na mazingira tunayofanyia kazi. suala la upandishwaji vyeo, kuthibitishwa kazini pamoja na huduma nyingine za kiutumishi ni jukumu la muajiri kuendana na miongozo iliyowekwa” Amesema Kisinza.

Miongoni mwa mada zilizofundishwa ni dhana ya Utumishi wa Umma sheria,kanuni,miongozo na taratibu, Misingi ya maadiliya utendaji kazi katika utumishiwa Umma,majukumu na wajibu wa Maafisa Watendaji wa Kata,Usimamizi wa miradi ya Serikali, Ukusanyaji na utunzaji wa mapato ya Serikali, Misingi ya utoaji huduma bora kwa wananchi pamoja na mbinu za Kimenejimenti ya udhibiti na utatuzi wa migogoro katika ngazi ya Kata na Mitaa.

Ikumbukwe kuwa tangu mwaka 1984, serikali iliporejesha mfumo wa serikali za mitaa, jitihada kubwa zimekuwa zikifanyika katika kujenga mfumo imara wa kitaasisi ili kusimamia na kuratibu shughuli za utawala, utendaji na maendeleo katika ngazi ya mkoa ,wilaya halmashauri,tarafa,kata,kijiji,mtaa na kitongoji.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.