Header Ads

RC MALIMA ,AONGOZA MAMIA YA WANANCHI KUADHIMISHA SIKU YA KUWAKUMBUKA MASHUJAA.



MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, ameongoza mamia ya wananchi katika kuwakumbuka mashujaa  walipoteza  maisha yao yao wakiutetea,Kuupigania na Kulinda  Uhuru wa Tanzania. 

Maadhimisho hayo yamefanyika Julai 25-2024 katika eneo la mnara wa Mashujaa jirani na Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza  katika sherehe hizo za kumbukizi ya Mashujaa,  RC Malima, amesema Mashujaa hao walipambana kwa hali na mali kwa ajili ya kuitetea Nchi ya Tanzania wakiwa katika Maeneo Mbalimbali.Walijizatiti na kujitoa  kwa uzalendo mkubwa kwa kuweka rehani Maisha yao kwa ajili ya Tanzania.

RC Malima , amesema  Mkoa wa Morogoro unaungana na  Watanzania wote kuwakumbuka na kuwaombea kheri kutokana na kujali na kudumisha Misingi ya Amani.

Aidha,RC Malima , amesema kuwa Misingi mizuri na imara iliyojengwa wasisi wa Taifa letu baba wa Taifa  ,Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere Na Sheikh Abeid Amani Karume,imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa Amani na Utulivu,huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote wa Ndani au Nje.Amani iliyojengwa na  imepelekea wageni,wakimbizi na watalii kuifanya Tanzania kuwa kivutio na kimbilio.

" Tuendelee kuienzi na kuilinda Amani ya Nch yetu.Wapo wanaosema Kuwa Amani ni sawa na Yai mkononi,ukilivunja hautaweza kulinganisha kamwe;wengine wanasema kuwa Amani  haina bei na ikipotea haina soko la kununu.Tuitunze Amani yetu" Amesema RC Malima .

Miongoni mwa shughuli zilizofanyika ni dua na sala maalum ya kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi kutoka kwa viongozi wa dini pamoja  gwaride maalum kwa ajili ya mashujaa.

Katika maadhimisho hayo, Manispaa ya Morogoro iliadhimisha kwa kufanya shughuli za kijamii ikiwemo kufanya usafi wa Mazingira katika eneo la JUWATA Stendi ya Bajaji Julai 24-2024.

Kila ifikiapo Julai 25 ya kila Mwaka,Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza Maisha yao wakiutetea,Kuupigania na Kulinda  Uhuru wa Tanzania. 


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.