KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI , ELIMU NA AFYA MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO
KAMATI ya Huduma za Uchumi, Elimu na Afya Manispaa ya Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wake , ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kingo, Mhe. Amini Tunda, pamoja na timu ya wataalamu ya Wakuu wa Idara na Vitengo imeeleza kuridhishwa na ubora wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika hatua tofauti tofauti katika Manispaa ya Morogoro.
Wajumbe wa Kamati hii wameeleza haya Julai 22-2024 katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Katika ziara hii, Wajumbe wametembelea na kukagua ujenzi wa madarasa mapya shule ya Sekondari Kingo pamoja na Shule ya Sekondari Nanenane, Hospitali ya Manispaa ya Morogoro , Zahanati ya Mji Mkuu pamoja na maboma ya madarasa Shule ya Msingi Misufini B Kata ya Mafiga.
Aidha, pamoja na kuridhishwa na ubora wa miradi hii ambayo kimsingi ipo katika hatua tofauti tofauti ya utekelezaji na mengine kuanza kutumika kutoa huduma , wajumbe wameshauri ujenzi wowote amabao bado haujakamilika ukamilike kwa wakati ili utoa huduma kwa wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya Kamati hiyo, Mhe. Tunda, ameishukuru sana Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipatia fedha za miradi ya maendeleo Manispaa ya Morogoro.
Post a Comment