Header Ads

KAMATI NDOGO YA MAZINGIRA MANISPAA YA MOROGORO YATAKA WANANCHI KUWAJIBIKA KATIKA USAFI WA MAZINGIRA KUWEKA MJI SAFI.

KAMATI ndogo ya Mazingira Manispaa ya Morogoro imewataka  watendaji wa Kata na Mitaa, wananchi pamoja na  wadau mbalimbali wa utunzaji wa mazingira kuhakikisha Mazingira ya Manispaa yanakuwa safi na kutunzwa muda wote.

Kauli hiyo, imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Diwani wa Kata ya Kihonda, Mhe. Hamisi Kilongo  Julai 18/2024 katika ziara ya Kamati hiyo ya kutembelea Kata ya Mji Mkuu na Mwembesongo  kuangalia maeneo ambayo yanawadhabuni wa taka na yale ambayo Kata husika wanatumia vikundi vyao vya ndani vya uzoaji wa taka.

"Tulikuwa na ndugu zetu Kampuni ya uzoaji taka Kajenjere na sasa hawapo tena na tumepata wadhabuni wapya kwenye maeneo yetu, kwahiyo ni niwajibu wa viongozi kusimamia suala la usafi wa mazingira, pia wananchi na  wadau wa mazingira lazima wawajibike katika utunzaji wa mazingira ili kuliweka Mji wetu wa Manispaa  katika hali ya usafi"Amesema Mhe. Kilongo.

"Mji wetu upo katikati, tuna miradi mikubwa sana ya kimkakati, ndoto yetu ni kuwa Jiji, hatuwezi kuwa Jiji kama Mji wetu utakuwa mchafu , tujipange sawasawa , tuhakikishe tunatunza mazingira ili iwe kama njia ya kuishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan,  kwa maendeleo waliyotufanyia”Ameongeza Mhe. Kilongo.

Kwa upande wa Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwembesongo  Mhe. Ally Kalungwana , amesema Kata yake wamejipanga vizuri kuhakikisha Kata hiyo inakuwa safi kwa kushirikiana na wadhabuni wa taka waliokuwepo.

Naye Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Mhe. Samweli Msuya , amesema Kata yake imejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wake wanahudumiwa vizuri hususani katika suala zima la uzoaji wa taka.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.