MWENGE WA UHURU 2024 WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI 3.6 MANISPAA YA MOROGORO
Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 Godfrey Mnzava, Aprili 27/2024 umezindua miradi 10 ambapo umeweka jiwe la Msingi, umekagua na kuona miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.6 Manispaa ya Morogoro.
Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa uhuru 2024 ni kuona shughuli za Kikundi cha Vijana cha kuchakata nafaka MOU AFRIKA kilichopo Kata ya Chamwino chenye thamani ya Milioni 35, Kuzindua mradi wa uboreshaji wa huduma za Maji Bilioni 1.7, kuona shughuli za upandaji wa miti na uhifadhi wa mazingira Bwawa la Mindu milioni 50, Kuona uendelevu wa mradi wa maji Kauzeni uliozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhutu 2023 milioni miloni 34.5, Kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Zahanati ya Kauzeni milioni 141.4 , Kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Kichangani milioni 474.9, Kuzindua mradi wa Shule ya Msingi Viwandani Shilingi Milioni 481.4, Kuona uendelevu wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Utawala Sekondari Mkundi ambalo limewekwa Jiwe la Msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 milioni 13.2, kufanya matendo ya huruma kwa walengwa wa Kituo cha Makundi Maalum MIHAYO na kuzindua Jengo la wafanyabiashara wadogo wadogo Machinga Complex lenye thamani ya milioni 639.4
Akiwa
katika mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kichangani, ameridhishwa na ujenzi huo
ambapo amesema kuwa mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Manispaa
ya Morogoro.
Pia amewataka wananchi kuishiriki kikamilifu katika uchaguzi wa
Serikali za Mitaa 2024 na kuwaacha
Viongozi waliopo madaraka kufanya kazi zao bila kusumbuliwa kwani muda wa
uchaguzi bado.
Post a Comment