Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO YAADHIMISHA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBARI KWA KUFANYA MAOMBI NA USAFI WA MAZINGIRA


WANANCHI na Wakazi wa Manispaa ya Morogoro   wameendelea na maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60  ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya Usafi na kufanya maombi kwa Viongozi walitangulia ambao walikuwa chachu ya kuweka misingi ya Muungani ambao ni aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa ZanzibarSheikh Abeid Amani Karume, tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar.

Maadhimisho hayo yamefanyika Kata ya Mafiga  Aprili 22, 2024  yakiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Emmanuel Mkongo.

Akiwa katika eneo la Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Kata ya Mafiga , Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Emmanuel Mkongo, amewataka Wananchi wa Manispaa ya Morogoro  wote kuendeleza umoja na amani ili kudumisha amani ya Nchi  

Mkongo, amewataka wananchi katika kuendelea kuenzi Muungano wa miaka 60, wananchi waendelee kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka, upandaji wa miti na kuhakikisha wanashiriki shughuli  mbalimbali za kijamii kwa ajili ya Maendeleo ya Manispaa na Taifa kwa ujumla.

Aidha,Mkongo amesema,  katika kilele cha Muungano, Manispaa ya Morogoro inaendelea na matukio mbalimbali kama usafi wa mazingira, upandaji wa miti ikiwa na lengo la kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Katika maadhimisho hayo ,  watumishi pamoja na jamii kwa ujumla wameshiriki katika  kufanya usafi maeneo yote ya Kata ya Mafiga husani katika kufyeka nyasi  maeneo ya barabara , Ofisi za Serikali na taasisi mbalimbali.

Katika kuadhimisha kilele cha Muungano , Manispaa ya Morogoro intarajia kufanya mahojiano na wazee maarufu wanajua historia ya muungano historia ya Mkoa wa Morogoro na Manispaa kwa ujumla  kabla na baada ya muungano ambapo mahojiano hayo yatakuwa na lengo la kufikisha ujumbe kwa Jamii juu ya umuhimu wa muungano huo na ulivyosaidia katika mambo ya uchumi, siasa na elimu.

Kilele cha maadhimisho hayo kwa upande wa Manispaa ya Morogoro katika sherehe za Muungano, itafanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege kuanzia majira ya saa 12;00 asubuhi.

Mara baada ya maadhimisho hayo kumalizika Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro ,Winfred Kipako,amechukua nafasi ya kuwaalika wananchi wote wa Manispaa ya Morogoro na nje ya Morogoro katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wa Kitaifa ambapo Manispaa ya Morogoro itakimbiza mwenge huo tarehe 27 mwaka 2024 mapokezi yake yakifanyika Uwanja wa mpira wa miguu Shule ya Sekondari Mafiga na kukesha Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege.

Ikumbukwe kuwa Tanganyika na Zanzibar iliungana April 26, 1964 na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.