Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako, akizungumza na wananchi waliohudhuria katika Siku ya Lishe na Afya Kata ya Mwembesongo.
Mtendaji wa Kata ya Mwembesongo, Amina Said, akizungumza na wananchi waliohudhuria katika Siku ya Lishe na Afya Kata ya Mwembesongo.
Mtendaji wa Kata ya Mwembesongo, Amina Said (wapili kulia) ,akizungumza na wataalamu wa Lishe na Afya kutoka Chuo Kikuu cha SUA.
AFISA Tarafa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako, ametaka wadau wa lishe kupambana kutokomeza udumavu ndani ya Manispaa ya Morogoro hususani wakazi wa Kata ya Mwembesongo ili kuwa na jamii bora isiyo na udumavu .
Kauli hiyo ameitoa leo Agosti 28/2021 katika uzinduzi wa Siku ya Lishe na Afya Kata ya Mwembesongo, iliyofanyika katika eneo la Ofisi ya Kata.
Akizungumza na Wananchi waliohudhuria katika siku hiyo ya Lishe , Kipako, amesema kuwa Manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa Manispaa ambazo hazina shida ya vyakula, hivyo si sahihi Kata ya Mwembesongo, ikawa na tatizo la udumavu wakati chakula kipo cha kutosha .
"Kwanini Mwembesongo tuendelee kuwa na uduamavu wakati tunalima matunda ya kutosha ,tuna wanga wa kutosha na mboga za majani za kutosha tuna kila aina ya virutubisho vya mwili tumekuwa na changamoto ndogo ndogo ambazo zilikiukwa toka zamani ila sasa ni wakati mzuri wa kuzifanyia kazi changamoto hizo " Amesema Kipako.
Aidha, amesema moja kati ya changamoto kubwa ya baadhi ya wazazi kutozingatia utunzaji mzuri wa watoto wakati wakiwa na ujauzito na baada ya ujauzito kwa kushindwa kulea watoto kwa kipindi cha siku 1000 kama inavyotakiwa kwa mtoto kutunzwa.
Kipako, amesema kuwa suala lishe limekuwa na tatizo mtambuka katika Taifa , hivyo ni wajibu kwa wadau wote ndani ya Kata ya Mwembesongo kupambana na suala la lishe .
Kuwa taifa linapokuwa na watu wengi wenye udumavu ni hatari sana kwa Taifa linakosa watenda kazi wazuri hivyo ni lazima kujipanga kuona suala la lishe linapewa kipaumbele kama njia ya kuondokana kabisa na changamoto ya lishe na udumavu ndani ya Kilakawilaya .
Hata hivyo, amesema hali ya lishe inapaswa kuongezwa zaidi ili kuona jamii inatumia vema vyakula vinavyo zalishwa katika Manispaa ya Morogoro hiyo kama sehemu ya kuongeza lishe bora kwa jamii .
Naye Mtendaji wa Kata ya Mwembesongo, Amina Said, amesema kuwa sababu kubwa inazosababisha hali hiyo ni kutowekeza muda wa kuwa na watoto kuwalisha ipasavyo ikiwepo kuwapa pombe kwa baadhi ya maeneo, lishe duni kutokana na wananchi kutokuwa na elimu ya ulaji wa chakula cha kutosha na chenye mchanganyiko wa viini lishe.Amina amesema , kuwa kuwa kutokana na changamoto hiyo, Kata ya Mwembesongo, inatarajia kuweka mikakati mbalimbali katika kuweza kupambana na hali ya utapiamlo na udumavu kwa watoto wenye chini ya miaka mitano ikiwemo kutoa elimu ya nadharia na vitendo kwa jamii kuhakikisha kwamba ulaji wa kiwango cha juu cha virutubishi unafanyika na kuzingatia unyonyeshaji katika siku 1,000 za mtoto unafuatwa.
Naye Mwananchi wa Kata hiyo, Juma Abdallah, ameupongeza Uongozi wa Kata ya Mwembesongo, kwa kuifanya Siku hiyo katika Kata hiyo.
"Tunampongeza Mgeni rasmi kwa kuacha majukumu yake na kujumuika na sisi kwa kweli leo tumepata elimu kubwa ambayo hatukuwa nayo tunaomba elimu hii isiishie hapa bali ifike kwa wananchi zaidi ili kila mtu anufaike " Amesema Abdallah.
Post a Comment