MASHINDANO YA WAGALA CUP YAZINDULIWA RASMI , YAJA NA MKAKATI WA KUSAKA VIPAJI KATA YA KIHONDA
DIWANI wa Kata ya Kihonda, Mhe. Ramadhani Myolele, amezindua mashindano ya WAGALA CUP 2026 , ambayo hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kuinua vipaji vya vijana na kuwasaidia kuondokana na matatizo yanayowakumba.
Mashindano hayo, yamezinduliwa katika Uwanja wa Don Bosco uliopo Kihonda huku timu 20 zikishiriki mashindano hayo.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Mhe.Myolele, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuwaweka karibu vijana ili waweze kuwa jamii moja kupitia soka, kujenga undugu na uraia na pia kuondokana na matumizi ya madawa ya kulevya.
“Nimeona kuja na mashindano haya kwa vijana, nategemea baada ya mashindano haya tuibue vipaji kwa vijana wetu, lakini mashindano haya ni moja ya utekelezaji wa ilani ya CCM kipindi cha uchaguzi wangu ,yenye lengo la kufufua vipaji vya vijana na nawashukuru waratibu na watu wengine ambao wamefanikisha zoezi hili" Amesema Mhe. Myolele.
Aidha, Mhe. Myolele, amewataka Vijana kucheza kwa nidhamu na kwa upendo kwani mashindano hayo kwani yanalengo la kubua vipaji vya vijana.
Kwa upande wa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kihonda, Inspekta. Edson Kitanda amempongeza Mhe. Myolele kwa hatau za kukuza vipaji kwani Morogoro imekuwa ni kitovu cha kuzalisha wachezaji wazuri na bora.
" Nipo hapa kushiriki, nimepata mwaliko , Mh.Myolele ni ndugu yangu na hiki anachokifanya ni moja ya utekelezaji wake katika kukuza michezo, niwapongeze na waratibu wengine pamoja na timu zote zilizokubali kushiriki mashindano haya" Amesema Inspekta. Kitanda.
















Post a Comment