EGG TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA SOMUNCU BABA WAFUTURISHA ZAIDI YA WATU 500
TAASISI ya EGG Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya SOMUNCA BABA , Machi 27-2025 limewafuturisha zaidi ya watu 500 kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo na Taasisi za UMMA na Binafsi.
Akizungumza mara baada ya iftari hiyo, Mkurugenzi wa EGG Tanzania, Sheikh Jumanne Mpinga, amesema katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani jamii haina budi kuwa na huruma kwa wale wasio na uwezo, ambao ni wajane na yatima ili kuwasaidia waweze kutekeleza ibada ya funga vizuri.
“Katika mwezi wa Ramadhani, tunahimizwa kuwa wakarimu na kuwasaidia watu wasio na uwezo kwani ni sehemu muhimu katika mwezi huu ili nao waweze kufurahia mfungo wa mwezi huu,” Amesema Mpinga
Mpinga, amehimiza umoja na mshikamano miongoni mwa wadau mbalimbali , Taasisi na jamii kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa karibu ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma.
Naye Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro, Mwal.Mussa Katunzi ameipongeza EGG Tanzania, kwa kuwaalika na kuwafuturisha watu kwani imeonesha ni jinsi gani wanajali makundi ya watu pamoja na kutengeneza upendo katika jamii.
Katunzi,amesema EGG Tanzania wamekuwa sehemu ya msaada mkubwa kwa jamii kwani katika Manispaa ya Morogoro wamefanikisha kuchimba visima kwa shule mbalimbali ili kuokoa adha wanazozipata wanafunzi kutokana na ukosefu wa maji.
Post a Comment