Dc
DC NSEMWA AONGOZA UPANDAJI WA MITI 3000 MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI MANISPAA YA MOROGORO.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Rebeca Nsemwa ameongoza mamia ya wadau wa Mazingira Manispaa ya Morogoro kupanda miti 3000 katika maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani Manispaa ya Morogoro.
Zoezi la upandaji wa miti hiyo ikiwemo miti ya matunda na mikarafuu limefanyika Juni 04/2024 Shule ya Sekondari Konga Kata ya Mzinga.
DC Nsemwa, amesema kampeni yake ya sasa ni kuhakikisha Shule zote za Wilaya ya Morogoro zinapanda miche ya mikarafuu isiyopungua 100.
" Tumepanda miti 3000, lakini maelekezo ya Mkoa wetu kipaumbele Cha kwanza kupanda miti ya mikarafuu, na hapa tumepanda miti 2000 ya matunda na tumegawa miti 1000 ya mikarafuu kwa Wananchi wa Luhungo,Mzinga na Milimani, tunataka mikarafuu hii iwe sehemu ya kuongeza vipato vyetu baada ya miaka 3, hata michango ya Wazazi ya chakula shuleni kama mikarafuu ikizaa tutapata fedha na shida zote za kuwabana Wazazi fedha ya chakula hazitakuwepo" Amesema DC Nsemwa.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amempongeza DC Nsemwa kwa mapambano yake ya kuitaka Morogoro kuwa ya kijani lakini kusimamia Mazingira kikamilifu kwa kupanda miti ili kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Mazingira, Mhe. Hamis Kilongo, amesema Manispaa ya Morogoro itaendelea kupanda miti na kutunza Mazingira Kwa kushirikiana na wadau wa Mazingira na kusimamia kikamilifu sheria ndogo ya Mazingira ya mwaka 2024 ili kuhakikisha Mji unakuwa safi na Salama.
Meneja NEMC Mkoa wa Morogoro, Abel Sembeka, amesema NEMC itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa Halmashauri zote Mkoa wa Morogoro ili kuhakikisha uhifadhi wa Mazingira unakuwa kipaumbele kwa Wananchi.
Miongoni mwa wadau wa Mazingira, kutoka Benki ya Diamond Trust Bank ( DTB Bank) , Meneja wa Masoko DTB Benki , Silvester Bahati , amesema DTB Benki wataendelea kusaidia shughuli zote za uhifadhi wa Mazingira kadri watakavyoweza kijadiliwa kupitia Bajeti zao na kuwa Benki namba moja ambayo itakuwa mstari wa mbele kuchochea uhifadhi wa Mazingira nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Dkt. Maneno Matawa, amewashukuru wadau wa Mazingira waliojitokeza huku akiomba ushirikiano huo uendeleee kwani adhima ya Manispaa ya Morogoro ni kuwa Jiji na hawawezi kuwa Jiji kama Mji bado ni mchafu.
Post a Comment