Header Ads

WATUMISHI OFISI YA MKUU WA MKOA MOROGORO WAPONGEZA JITIHADA ZA RAIS DKT SAMIA KUWEKA MAONESHO YA SABABSA KATIKA VIWANGO VYA KIMATAIFA



WATUMISHI kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuyafanya maonesho ya sabasaba ya 49 kuwa katika viwango vya Kimataifa na kuwavutia wawekezaji kuwekeza nchini.

Hayo yamesemwa na baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakati wakitemebelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Sabasaba ya 49 Julai 7-2025.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi hao, Msimamizi wa Ofisi ya Masijala kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Foida Kikoti wakati wa kutembelea mabanda hayo ya maonesho.

Aidha,watumishi hao wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.

Pia,watumishi hao wameipongeza Tan Trade na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  kwa kuendeleza maonesho hayo na kuyaweka katika viwango vya Kimataifa.

Wakiwa katika upande wa Ofisi ya Waziri Mkuu,wamesema wamejifunza mambo mengi ikiwemo majukumu na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu -Sera, Bunge na Uratibu , Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi,Ajira ,Vijana na wenye ulemavu pamoja na taasisi mbalimbali zilizo chini ya Ofisi hiyo.

Katika Ofisi hiyo, pia wameweza kujifunza namna ya uandaaji wa kikokotoo cha kustaafu kinavyopatikana pamoja na huduma zinazotolewa kwenye upande wa kitengo cha maafa.

Pia, wameweza kutembelea katika mabanda ya wanawake wajasiriamali na kujionea ubunifu pamoja na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake hao.

Wakiwa katika Banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wamesema wamejifunza namna ya kutambua uwizi wa mitandaoni, kujua usajili wa laini za simu, kubaini matapelei wa njia za mtandao pamoja na kupunguza matumizi ya vifurishi katika simu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.