Header Ads

BONANZA LA MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR LAFAANA


KATIKA Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Wananchi wa Wilaya ya Morogoro  wameshiriki michezo mbalimbali katika kuadhimisha sherehe hizo.

Michezo hiyo imefanyika Aprili 26-2025   katika Kiwanja cha Mpira shule ya Msingi  Mwere  iliyopo Kata ya Kingo ikijumuisha michezo ya mpira wa Miguu , Netball na kuvuta kamba.

Kabla ya michezo hiyo kufanyika,sherehe hizo zimeambatana  na zoezi la upandaji wa Miti pamoja na ufanyaji wa usafi wa mazingira.

Katika upandaji wa Miti, jumla ya miti 71,000,013 imepandwa katika maeneo mbalimbali ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa michezo hiyo, Afisa Tawala Wilaya ya Morogoro akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Ndg. Hilary Sagara,  amesema kuwa michezo ni afya  hivyo katika kilele cha maadhimisho hayo ni  muhimu kuimarisha afya ili kuendelea kuleta maendeleo.


“Michezo ni afya  hivyo katika maadhimisho haya,  tumeona ni vyema tukawa na michezo ,kwanza inakutanisha jamii, kubadilishana ubunifu wa kiutendaji lakini michezo inaimarisha afya zetu"Amesema Sagara.


Katika hatua nyengine, Sagara,amesema mwakani watahakikisha kunakuwa na michezo mingi zaidi ya hii ambayo imefanyika kwani zipo changamoto walizoziona na watazifanyia kazi katika maadhimisho yajayo mwakani 2026.

Katika michezo hiyo, timu ya Mpira wa miguu ya Moro Heroes wameibuka washindi kwa mikwaju ya penati ya 5-4 dhidi ya timu ya Moro Star.

Kwa upande wa Netball,timu ya wanawake ya Moro Queen imeibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 31-10 dhidi ya timu ya Moro Manispaa.

kwenye mchezo wa Kuvuta kamba, timu ya wanawake Moro Queen waliibuka kidedea kwa kuwavuta timu ya wanawake Moro Manispaa na upande wa wanaume,timu ya Moro Heroes iliwashinda timu ya Moro Star.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.