HUMANITY FIRST TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA AHMADIYYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA YAIKABIDHI SERIKALI YA MKOA WA PWANI TANI 7.5 ZA CHAKULA KWA WAHANGA WA MAFURIKO
SHIRIKA la Humanity First Tanzania (Utu kwanza) kwa kushirikiana na Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania, wameikabidhi Serikali ya Mkoa wa Pwani jumla ya tani 7.5 za chakula kwa ajili ya kusaidia Kaya 125 zilizo athirika na mafuriko yaliyotokea Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani.
Tukio hilo la kukabidhi vyakula hivyo limefanyika Mei 17/2024 ambapo mara baada ya kukabidhi vyakula hivyo waliungana na viongozi wa Mkoa wa Pwani kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na Mafuriko na kushuhudia uharibifu mkubwa ambao umezikumba familia mbalimbali na kusababisha wananchi kuondokewa na makazi na mali zao.
Aidha, waathirika hao wa mafuriko kwa nyakati tofautitofauti walipongeza Humanity First na Ahmadiyya kwa moyo wa kuwakumbuka
Akizungumza mara baada ya kufika katika Kambi waliyohifadhiwa waathirika hao wa mafuriko, Mratibu wa Shirika la Humanity First Tanzania Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya utoaji wa misaada mbalimbali katika Majanga kwa niaba ya Mwenyekiti wa Humanity First Tanzania, Shekh Abid Mahmood, amesema wametoa msaada huo kama kuwashika mkono waathirika wa mafuriko.
'Tumeguswa sana na matukio haya,tumeamua kukodi Mashua kufika hapa kujionea uharibifu, kama shirika ambalo kazi yake imekuwa ni utoaji wa misaada mbalimbali katika majanga tumeona tufike hapa, na hii ni awamu ya pili, awamu ya kwanza tulifika na kutoa tani 4 za chakula na sasa tumeleta tena Tani 3.5 za chakula, sote tupo pamoja katika wakati huu mgumu , tunawashukuru sana wote ambao wameguswa katika kutoa misaada kwenu" Amesema Sheikh Mahmood.
Miongoni mwa vyakula ambavyo Shirika la Humanity First Tanzania Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya utoaji wa misaada mbalimbali katika Majanga limetoa nia Unga wa mahindi, Maharage pamoja na sukari.
Post a Comment